BENI

DRC WATU WATATU WAUWA KWA MAPANGA KATIKA KIJIJI CHA MUNDU BIENA KATIKA MJI WA BENI.

MACHI 18, 2024
Border
news image

Taarifa kutoka muandishi wa MTV DRC ONLINE zasema watu tatu wamefariiki Dunia baada ya kuwawa na watu wanao dhaniwa kutoka kundi la kigaidi la ADF katika Mji wa Beni Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo ,miongoni mwa walio uwawa akiwemo askari mmoja wa POLISI katika la MUNDU BIENA Kata Sayo.

Wakaa wa Kata husika ya SAYO wasema kuna mlio wa risasi ulkio sikika katika kata hiyo ya Mji wa Beni Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo kwa saa za usiku na baadae kuwakuta watu wameuwawa wengine kwa kukatwa na mapanga.

Mauaji ya aina hii hutokea mara kwa mara katika Mji wa Beni na wilya zake ,vyombo vya usalama vikisema ni waasi wa ADF wanao husika ,ADF ina makamanda wake kutoka taifa la Uganda ,na wapiganaji kutoka mataifa yote ya Africa mashariki ,ikiwa ni mchanganyika wa watu wanao tekwa kwa nguvu wengi bila hiari yao.

Hivi karibuni ADF ilivaamia kambi ya Kakwangura Katika Mji wa Butembo na kuwabeba wafungwa Zaidi y amia nane (800) Pamoja na wengine katika Jela la kwangwayi mjini Beni . ADF ikifanya hivyo katika katika uangalizi wa vyombo vya ulinzi na usalama hata kikosi cha umoja wa Matifa MONUSCO. Kuna vitendo vingi ambavyo watu hujiuliza kweli ni ADF inayo fanya hivyo ama mabandia wengine. Mashambulizi ya ADF ikizusha wasiwasi kote Beni Mjini na wilayani.

AM/MTV DRC ONLINE.