TANZANIA

DRC WANAWAKE WAOMBA WAZIRI MKUU KUJIKITA KATIKA KURUDISHA USALAMA MASHARIKI MWA CONGO KWA HARAKA.

Aprili 03, 2024
Border
news image

Siku chache baada ya kuteuliwa kama Waziri mkuu wa Congo DRC katika histori ya taifa hilo.wanawake waomba Judith Tuluka kufanya liwezalo kurejesha amani kote mashariki mwa Congo hasa kumaliza vita na kuwarudisha nyumbani wakimbizi wote wanao zunguuka mji wa Goma kutokana na uasi wa M23 .

Josephine Malimukoni mmoja wa watetezi wa haki za wanawake mashariki mwa taifa La congo DRC asema Kuna matatizo mengi sana DRC ila kinacho hitajika kwa haraka ni amani na usalama kwa wakaazi wa Kivu kaskazini na Ituri ambako kuna shuhudiwa maafa makubwa ,hasa mauaji na kulazimisha wakaazi kukimbia vijiji vyao kutokana na ukosefu wa usalama.

Malimukono anasema .Waziri mkuu akiwa akina mama awe tafauti na wengine hasa kuepuka Rushwa na kujipenelea bali atazame hali wanayo pitia wanawake na watoto klatika kambi mbali mbali zinazo zunguuka mji wa Goma .

Vita mashariki mwa Congo vimesabisha wanawake kuwa wagonjwa wa ukimwi kutokana na hali ya ubakaji wa mara kwa mara ,ubakaji unao tekelezwa na watu wenye silaha katika kambi ama pembezoni mwa Kambi .wengi wao waliacha vijiji vyao na kwa sasa wakimbizi katika taifa lao kutokana na vita vya M23 na serikali ya Congo DRC.kwa sasa wakiwa kambini bila chakula,dawa n ahata ukosefu wa mavazi.

AM/MTV DRC ONLINE