DRC

DRC Wakimbizi wa Vita mashariki mwa Congo waomba kurejea nyumbani kutokana na mateso wanao pitia katika kambi mbali mbali .

Aprili 24, 2024
Border
news image

Wakishudia mvua kali kwa sasa katika hema zao ambako waishi katika kambi mbali ,wakimbizi wa vita mashariki mwa Congo waomba kurejeshwa kwenye vijiji vyao kwani wamechoka na Maisha ya kuishi katika hema . Mmmoja wa wkaimbizi alie hifadhi jina lake asema ,kwa sasa amejikuta na maradhi ya msongo wa mawazo kutokana na Maisha anayo ishi kwa sasa akiwa na Watoto kambini bila kusoma . Mama huyu anasema kila siku anaondoka asubui kambini kutafuta kuni katika mbuga la Wanyama pori la Virunga pembeni ya kambi yake ya Bulengo lakini hukutana na watu wenye silaha wanao baka wanawake.

Ubakaji wa wanawake,ukosefu wa Chakula na ukosefu wa Tiba imekuwa shida na tatizo kubwa kwa wakimbizi wa Vita mashariki mwa Congo ,hasa katika kambi zinazo zunguuka Mji wa Goma ambako wengi waishi katika hema bila kupewa msaada wa Chakula .mmoja wa akina mama anae kuwa na Watoto sita asema kwa sasa ana miezi sita bila kupata chakula japo wengine wamekuwa wakipata angalau msaada mdogo ja hautoshe.

Wakimbizi wa vita kwa jumla wakiomba amani na usalama kwenye vijiji vyao ili warudi na kuanza masisha mapya kwenye vijiji vyao ambako watalima chakula kuliko kubaki wakiomba masaaada wa chakula isio patikana ,na Watoto wao wakibaki bila elemu asema mama mmoja akiangusha machozi . Setikali ya Congo imekuwa ikiwapa Moyo wakimbizi kwamba jitihada zinafanyika ili usalama urudi kwenye vijiji vyao na ili warudi. Gavana wa Kivu Kaskazini Meja Generali Peter Cirimwami alikuwa akisema kwamba Rais wa Congo anafanya jitihada zote kwakurejesha amani na usalama kwa wakaazi wa Masisi,Rutshuru na Nyiragongo ili warudi nyumbani kwao.

Wana diplomasia wakiomba Mzozo wa Congo umalizike kwa njia ya diplomasia kuliko utumia wa silaha swala ambalo hadi sasa serikali haijakubali ,hasa Mazungumuzo na kundi la M23 .

AM.MTV DRC ONLINE