DRC

DRC /WAFUNGWA KATIKA GEREZA KAKWANGURA MJINI BUTEMBO WALALAMIKIA HALI NGUMU NA MBAYA YA MASIHA .

Aprili 03, 2024
Border
news image

Wafungwa katika gereza ya Mji wa Butembo Kivu kaskazini mashariki mwa Congo wasema hali ni ya kutatanisha ,hali ambayo imesababisha vifo vya watu wengi kwa sasa kati mwezi mmoja watu wakifariki Dunia kutokana na ukosefu wa dawa na chakula na huduma nyingine muhimu. Kakwangura ni gereza ya watu wa chache lakini kwa sasa ikiwa na idadi kubwa kuliko ya kawaida ,wafungwa wakiishi bila chakula na hata wakishuhudia ukosefu wa chakula na dawa.

Hali kama hii hushudiwa kote nchini DRC ambakob Gereza huitwa njiabya kifo kutokana kwamba ukifungwa hakuna msaada wowote wakukijia ,baadhi ya wafungwa wakisema wamewekwa gerezani bila kusikilizwa na mahakama na kufahamu hatima yao.wengi wakifungwa bure ama kwa deni ndogo lakini waki na Zaidi yam waka mmoja gerezani bila kusikilizwa.

Gereza kadhaa nchini DRC zina shuhudia ukosefu wa chakula ,dawa,choo nzuri na hata huduma nyingine na wingi wa watu gerezani kuliko idadi kamili inayo pelekea msongamano na kusababisha vifo. Wafungwa wakipata msaada kutoka watu binafsi ,kanisa na watu wenye roho njema ,japo ni majukumu ya serikali kuwalisha wafungwa hao. Gereza nchini DRC ni njia moja ya kifo wasema wafungwa walio wahi kungia gerezani na kuachiliwa baadae.

AM/MTV DRC ONLINE