DRC

DRC UJENZI WA BARABRA BUTEMBO BENI

JANUARI 30, 2024
Border
news image

Gavana kwa muda wa Kivu Kaskazini peter CIRIMWAMI akwenda mwendo Kasi katika Miradi ya maendeleo katika Mkoa wake unao taabishwa na ukosefu wa usalama.

Akizungumuza na waandishi hapa katika Miji ya Beni na Butembo gavana wa Kivu Kaskazini kwa muda asema maendeleo ni muhimu japo Mkoa wake unashuhudia mapigano makali kati ya M23 na jeshi la serikali wilayani Masisi ,Rutshuru,Nyiragongo na sehemu moja ya walikale ,mapigano inayo sababisha maelfu ya wakaazi kuhama nyumba na vijiji vyao .

Akiwa ziarani kwa siku Tatu katika katika Miji ya Butembo na Beni CIRIMWAMI amezindua miradi kadhaa ikiwemo ujenzi wa barabara,unjenzi wa uwanja wa ndege,barabara mbau Kamango ,ujenzi wa barabara Malepe Mjini Beni ,na barabara Nyamwisi katika Mji wa Butembo. Katika mji wa Butembo Gavana alikutana na kundi mbali mbali za kiraia wengi wakiomba usalama kuliko maendeleo ,lakini gavana aliwajibu kwamba vita haiwezi kwamisha shughuli za serikali kwani kusimamisha maendeleo itakuwa ni tatizo kubwa.

Vijana wakiomba kushirikishwa kwa haraka katika usalama hasa kujiunga na wazalendo kwazuia waasi wa M23 kuingia katika Mji wa Kanyabayonga wilayani Lubero.akina mama kwa uapande wao wakiomba usalama wa wanawake na Watoto kuimarishwa ili warudi kwenye vijiji vyao. Kwa upande wake PETER CIRIMWAMI nikwamba Rais wa Taifa anafanya liwezalo kuhakikisha usalama unapatikana kwa njia zote hasa za kijeshi.

Wakaazi wa vijiji vya Nyanzale,Rwindi ,Kibirizi ,Chirima na sehemu nyingine wakilazimika kuhama vijiji vyao kufatia mapigano ya M23 na jeshi la serikali na vijiji vyao kutekwa na waasi wa M23 ikiwemo SOMIKIVU kiwanda cha Madini.

AM /MTV DRC ONLINE