DRC

DRC SERIKALI YA CONGO DRC YAWAPA MSAADA WA CHAKULA FAMILIA ELFU ARBAINI NA SITA KUTOKA SAKE NA SHASHA KIVU KASKAZINI.

MACHI 13, 2024
Border
news image

Akizungumuza na na wanahabari katika kambi moja ya lac vert magaharibi mwa Mji wa Goma PRISCA LUANDA mshahuri wa gavana kwa maswala mbali mbali hasa Kiutu ,Afia na msemaji wa Gavana wa Kivu Kaskazini anasema Familia Zaidi ya elfu arbaini zote kutoka Mji wa Sake,Shasha na vijiji vingine ndio watafanikiwa kupata msaada huo wa Unga,maharagwa ,wengi wao wakiwa na mwezi mmoja bila chakula wakilala kambini katika matatizo mwenge.

Wakaazi walio pokea msaada huo wakionekana na furaha kubwa ikiwa mara ya kwanza kwao kupata chakula ,Justine ni mama alie kuwa amefanya siku mbili bila chakula anasema msaada huo utsaidia kidogo kuwalisha Watoto wake ila anacho hitaji Zaidi nikuona serikali imerejesha usalama kwanye vijiji vyake kwani hana inamani ya kutegemea misaada kwani ana shamba za kutosha kwenye vijiji vyake.

Wakaazi hao wote kwa jumla waomba Rais wa Taifa kuwapa usalama kwenye vijiji vyao kwani kutegemea Msaada haita saidia lolote kwa Maisha yao wakaazi hao wengi walikimbia mapigano makali inayoendelea kati ya M23 na jeshi la serikali wilayani Masisi na wengine wilayani Rusthururu ,sehemu nyingine ikiwa wilayani lubero ambako wapitia hali ngumu na mbaya ya kimaisha.prisca anasema msaada ulio tolewa na serikali umekabidhiwa kwa shirka la CARITAS ya Congo kwa ajili ya ugawanyazi sahihi na bora.

Wakaazi wengi kwa sasa wabaki hata bila hem ana vibanda kwa Watoto wao.

AM/MTV DRC ONLINE.