DRC

DRC RUTSHURU: MAPIGANO MAKALI KATI YA M23 NA WAPIGANAJI WAZLENDO KARIBU NA KIBIRIZI WILAYANI RUTSHURU KIVU KASKAZINI MASHARIKI MWA CONGO.

Aprili 04, 2024
Border
news image

Kwa mjibu wa wakaazi wa kiwanja na nyanzale nikwamba Mapigano makali yame ripotiwa tangu asubui hii tarehe nne April elfu mbili ishirini nan nekilometa sab ana Mji wa Kibirizi wilayani Rutshuru ,milio ya risasi kutoka silaha nzito na rasharasha .

Mulio wa risasi ukiendelea kwenye vijiji vya Kitolu na Kisingiri karibu na mji wa kibirizi wilayani ambao upo mikononi mwa waasi wa M23 wanao ungwa na jeshi la Rwanda serikali ya Congo ikisema .mapigano inayoendelea kati ya waasi na wapiganaji wazalendo ambao wengi wao ni vijana kutoka eneo mbali mbali wakipigania kila wanacho kiita uvaamizi wa vijiji vyao.

Baadhi ya raia wanaoishi pembezoni na mji wa kibirizi wasema ni tangu asubui ndipo walisikia murio wa risasi nakuanza kimbia makaazi yao kuhufia Maisha kwani wakati wa mapigano wengi hupoteza Maisha .

Utafahamu kwamba mapigano mengine yaliripotoka hapo jana katika eneo la Rwindi ambako wazlendo waliendelea kutwangana na M23.M23 ilio tangaza hapo majuzi kwamba itaenelea na mapigano yake hadi kuigomboa taifa lote la Congo akisema Nanga kiongozi wa waasi mashariki mwa Congo kwa sasa .

Nanga alisema baada ya Rutshuru atakwenda Butembo ,Beni na Ituri na Vile mjini Goma ,kwakuondoa serikali iliopo kwa sasa akisema Nanga katika mkutano na wakaazi wa Mji wa Rutshuru. Mapigano kati ya M23 na serikali ya Kinshasa imesababisha vifo ,mnaafa na uharibifu wa mali na vitu vya wakaazi ambao wengi kwa sasa wako katika kambi za wakimbizi pembezoni mwa Mji wa Goma katika kambi mbali mbali ambako wakimbizi hushudia milio ya risaisi kila jioni karibu na kambi zao ambako hawana msaada wa chakula Dawa na mavazi.

Wakaazi mashariki mwa Congo wameomba Waziri mkuu mpya ambae ni mama kufanya jitihada zote kumaliza vita mashariki mwa Congo na watu kurudi kwenye vijiji vyao.

Nadège Mulemba.