DRC

DRC OLIVE LEMBE KABILA AOMBA MUMEWE KURUDI MADARAKANI KWA HARAKA .

Aprili 02, 2024
Border
news image

Akiwa ziarani mashariki mwa Congo kwa Zaidi ya wiki moja ,Olive Lembe Kabila muke wa JOSEPH KABILA Rais mustaafu wa Congo asema kwa sasa inabidi mumewe arudi kwa haraka madarakani kuzima hali ya ukosefu wa usalama inayoendelea Kivu Kaskazini na kusababisha maelefu ya watu kuwa wakimbizi katika Taifa lao.

Lembe amesema kwa sasa ombi lake kubwa analo lifanya kila siku nikuomba Mumewe kurudi katika siasa na kuchukuwa uongozi wa Congo kuiokoa katika shida na kuwanusuru wakaazi walieko matatani wakipitia hali ya sintofahamu asema OLIVE LEMBE akiwa katika kambi moja ya bulengo Mjini Goma ambako waligawa kisaada ya vikwembe kwa wanawake wakimbizi.

Hadi sasa upande wa chama tawala haujasema lolote kuhusu msimamo huo kwani Congo DRC ipo katika demikrasia.kwa sasa upande wa Rais Mustaafu umekuwa ukikemea sana hali ya uongozi wa Felix Tshiskedi hasa swala la vita mashariki mwa Congo Kivu Kaskazini ambako uasi wa M23 umeungwa Mkono na Nanga ambae alikuwa kiongozi wa zamani wa Tume huru ya uchaguzi .

Nanga alikuwa mutu wa karibu wa chama cha PPRD na kwa sasa akishawishi wanasiasa wengi kijiunga na M23 .watu kutoka PPRD tayari wakiwa wamesha wasili wilayani Rutshuru kujiunga na Muungano huo wa M23 inayo twangana na Felix Tshisedi katika kile wanacho kita ukombozi.

Felix Tshisekedi wa Congo amaekuwa akisema hawezi zungumuza na M23 kwani ni vibaraka vya Taifa la Rwanda .vijana kadhaa wakiwa wamesha simama na kujiunga na makundi ya wazalendo ambao wanaunha mkono serikali kupigana na wale wanao sema ni wa vaamizi wa ardhi yao Kivu Kaskazini mashariki mwa Taifa la DRC.

AM/MTV DRC ONLINE