DRC

DRC MJI WA NYANZALE KUTEKWA NA WAASI WA M23 WILAYANI RUTSHURU KIVU KASKAZINI

MACHI 06, 2024
Border
news image

Wakaazi wa Mji Jirani wa Kibirizi wamelazimika kukimbia mkaazi yao na kukimbilia wilaya Jirani ya lubero,wengi wao wakiwa wanawake na Watoto wakikimbia na mizigo yao mgongoni na kutembea safari ndefu kwa mguu. Wakaazi hao wanasema wamelazimika kuhama makaazi yao kuona kwamba jeshi la serikali limeshindwa kuwarudisha nyuma waasi wa M23 ambao wamechukuwa vijiji vingi ,hasa NYANZA,Ngoroba,Kasyalira na vingine .

Shadrack MAFULA mmoja wa vijana katika Mji wa Kibirizi anasema wkaazi wana hathira kubwa kuona serikali ya Congo imeacha M23 kuchukuwa vijiji vyao katika uangalizi wa Umoja wa Matifa MONUSCO na kikosi cha SADEC ambacho kiliwasili Kivu Kaskazini siku zilizo pita.MAFULA amesema watu wengi wamehama makaazi yao na kukimbilia wilaya jiarani la Lubero hasa Katika Mji wa Kanyabayonga kuhufia Maisha ,wakaazi hao wakiwa Bila msaada wowote hadi sasa wengi wao wakiwa wanawake na Watoto.

Akitembelea wakimbizi wa Nzulo magharibi mwa mji wa Goma SHABANI akiwa mshahuri wa Rais Felix Tshisekedi amesema kilichoko kwa sasa nikuwa mkuu wa taifa la Congo anafanya jitihada zote kuhakikisha usalama wa wananchi unapatikana kwa njia zote hasa vita kwani mazungumuzo imechosha raia wa DRC.lakini vile Vita vime pelekea wakaazi wengi kuwa wakimbizi katika taifa lao na kwa sasa wakipitia hali ngumu katika kambi mbali mbali.

AM/MTV DRC ONLINE