DRC

DRC MAPIGANO MAKALI YA RIPOTIKA KATI YA WAASI WA M23 NA JESHI LA SERIKALI FARDC KARIBU NA NYANZALE WILAYNI RUTSHURU KIVU KASKAZINI MSHARIKI MWA CONGO DRC .

MACHI 04, 2024
Border
news image

Ni tangu asubui mapema milio ya silaha nzito na rasha rasha ilianza kusikika kwenye eneo za Kirima Bwito ambako waasi wa M23 waliamkia kushambulia kambi mbali mbali za jeshi la Congo AFRDC ,mapigano ambayo yaomekena kuwa makali.

Mapigano ambayo imewalazimisha wakaazi kuhama makaazi yao wakiwemo wanawake na Watoto wakikimbia na mizigo a wengine mbuzi ,mamama mmoja alie hifadhi jina lake asema kwa sasa wamechoka na hali ya ukimbizi wa mara kwa mara kwenye vijiji vyao wakipoteza vitu na mali yao n ahata kuacha shamba zao.mama huyu akibeba Godoro mgongoni asema mapigano ya muda mrefu kwenye vijiji vyao imesababisha familia nyingi kubaki fukara.

Mapigano mengine yakiripotiwa kwenye kambi mbali mbali ikiwemo barabara Mabenga ,barabra SOMIKIVU na nyanzale ,jeshi la Congo FARDC eneo hilo likisema bado laendelea kutwanga na kukabiliana na uchokozi wa waasi wa M23 ambao serikali inasema wanasaidiwa na jeshi la Rwanda hata wengine kutoka Uganda.M23 ikiendelea kuomba mazungumuzo na serikali ya Kinshasa swala ambako Rais wa Congo Felix Tshiskedi amesema kwa mara kadhaa kwamba hawezai kuzungumuza na M23.

Mapigano hayo yanajiri simu moja baada ya wakuu wa majeshi kutoka SADEC kumaliza ,mkutano wao katika Mji wa Goma ambako wamekubaliana kuongeza nguvu kwa ajili ya kukabiliana na makundi ya waasi mashariki mwa Congo hasa lile la M23 ambalo ni tishio kubwa kwa serikali.

AM/MTV DRC ONLINE