DRC/BENI

MAPIGANO MAKALI YASHUHUDIWA KATI YA SHEJI LA FARDC NA KUNDI LA ADF KATIKA KIJIJI CHA NGITE WILAYANI BENI kIVU KASKAZINI.

FEBRUARI 15, 2024
Border
news image

Akizungumza na MTV DRC ONLINE mmoja wa makamanda wa jeshi la serikali ya DRCongo wilayani Beni asema Mapigano kati yao na wapiganaji kutoka Kundi la ADF yameshuhudiwa usiku wa Jumatano hadi Alhamisi Februari 15, 2024 Katika Kijiji cha Ngite Kaskazini mashariki mwa Mji wa Beni karibu na Mji wa Mavivi na Mbau wilayani Beni, Ngite ni kijiji kinacho patikana takriban kilomita 15 kutoka mji wa Beni kwenye Barabara ya Kitaifa nambari 4 katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Msemaji wa jeshi eneo la Beni Kapteni Antony Mwalushayi wa Sokola 1, ana sibitisha habari hio, nakusema kwamba ADF ilikua Katika jaribio la kutafuta chakula na dawa kwa wapiganaji wake ndipo walianguka katika doria ya jeshi tiifu kwa serikali.

Kulingana na afisa wa kijeshi, mpiganaji mmoja wa ADF aliuawa kwenye uanja wa vita na mwingine mmoja tekwa na jeshi la Congo wakati wa mapigano makali vikali.

Utafahamu kwamba shambulio nyingine la ADF lilishuhudiwa Jumanne Januari 23, 2024 katika kijiji hicho cha Ngite, ambako watu watu waliuwawa .wilayani ya Beni imeshuhudia machafuko kwa muda mrefu na kusababisha watu wengi kubaki mayatima na wajane.

Germain Hassan KYAHWERE/Mtv DRDC online.