DRC/BENI

KIONGOZI WA WAPIGANAJI KYANDENGA AKAMATWA NA JESHI LA SERIKALI LA FARDC MASHARIKI MWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO.

FEBRUARI 16, 2024
Border
news image

Msemaji wa jeshi eeneo la Beni kapteni ANTONY MWALUSHAYI MBOMBO wa operesheni za kijeshi sokola1 ametangaza Katika barua Pepe kwamba vikosi vya ulinzi vya DRC vime mkamata kiongozi wa kundi la wa piganaji mayi-mayi KYANDENGA wilayani mambasa mkoani ITURI kunako umbali wa kilometa miamoja hamsini (150 )kusini mwa Mji BUNIA. KAMBALE MATABISHI maarufu PROF Ali tekwa wakati wa operesheni maalimum ilio endeshawa na jeshi tiifu kwa serekali ya Congo FARDC Magharibi mwa BIAKATO;taarifa zilizo fikia MTV DRC ONLINE zasema kama wa wapiganaji wa Kyandenga alikua amechukua uongozi wa muungano wa kundi moja linalo kuwa na uhusiano na magaidi wa ADF .Tangu kuKamatwa kwa kiongozi wake JEAN BAPTISTE KUPAKU maarufu KYANDENGA Katika Mji wa BUTEMBO septemba 18,2022.

Uta fahamu kwamba ADF imekuwa na ushirikiano na kundi la kigaidi la islamic state ambako lina watu wengi Duniani na Africa ambako wamekuwa wakitekeleza shambulizi na mauaji ya kinyama katika mataifa mbali mbali ikiwemo mashariki mwa Congo katika eneo la Beni chini yam ilima ya Rwenzori na wilayani Mambasa mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa Congo. Adf inashutumiwa kuwaua watu na kuchoma nyumba za watu wilayani Beni ambako wakaazi wamesha lazimika kuhama vijiji vyao .

Mauaji inayo fanyika katika uangalizi wa Umoja wa Matifa MONUSCO ambao wana kikosi kikubwa wilayani Beni kinacho kuwa na Ngome zake Katika Mji wa MAVIVI. Jeshi la Congo FARDC na lile la Uganda UPDF limekuwa likipambana na wapiganaji hao kwenye misitu ,wengi wao wakifariki Dunia na wengine kukamatwa.Ni Zaidi ya miaka kumi sasa ADF kuenelea na mauaji Pamoja na mashambulizi ya vijiji na miji wilayani Beni Kivu Kaskazini na mambasa Mkoani Ituri.

Germain Hassan KYAHWERE, MTV DRC ONLINE.