DRC

DRC /HALI YA WASIWASI MIONGNI MWA RAIA KUFATIA TISHIO LA WAASI WA M23 WANAO ONGOZWA NA NANGA KUTANGAZA KUINGIA GOMA KIVU KASKAZINI.

Aprili 01, 2024
Border
news image

Wakaazi wa Mji wa Goma,Beni Kivu Kaskazini Pamoja na Bunia Mkoani wa Ituri waishi wasiwasi kwa sasa kila siku kukicha kutokana na msimamo wa kiongozi wa M23 kutishia kuingia Goma .wiki ilio pita M23 ikiongozwa na NANGA alie kuwa kiongozi wa tume huru ya uchaguzi siku zilizo pita na kwa sasa akiwa kiongozi wa Uasi wa M23 mashariki mwa Congo kutangaza kuendelea na mashambulizi katika Miji na mikoa mbali mbali Mashariki mwa Congo.

Nanga alikuwa mgombea wa Kiti cha Uarais kwa uchaguzi ulio fanyika Decemba ilio pita na kwa sasa akiwa katika uasi wa M23 ambao una pata msaada wa kijeshi na chakula toka Mataifa Jirani ya Congo hasa mataifa inayo pakana na DRC eneo lake la Mashariki.Nanga ni raia wa Congo alie zaliwa Mkoa wa Isiro na kwa sasa akiwa Mpinzani makali wa uatawala wa Felix Tshisekedi kwa sasa ,sababu kubwa ya upinzani wake ikiwa haijulikani .

Uasi wa M23 umepingwa vikali na wakaazi wa mashariki mwa Congo waki lalamikia kile wanacho kiita uvaamizi na wizi wa madini na kutaka kulivaamia ardhi ya Congo .uasi huo ukiendelea katika uangalizi wa jumhia ya kimataifa ,yaani MONUSCO,SADEC na Hata Jumhia ya Africa Mashariki ambao wakaazi wa washutumu kuunga mkono uasi huo kidiplomasia na kiunafiki .

Mapigano ya M23 na jeshi la Congo imesababisha janga kubwa la kibinaadamu ,wanawake na Watoto wakiishi Maisha magumu katika kambi mbali mbali zanazo zunguuka Mji wa Goma na wengine wakipatikana eneo za Masisi ,Walikale na Lubero ambako wapitia hali ngumu ya Maisha kutokana na ukosefu wa chakula ,dawa na mahitaji mengine muhimu.

AM/MTV DRC ONLINE