DRC/GOMA

Gavana wa Kivu kaskazini PETER CIRIMWAMI aomba waty wote wanao miliki silaha kuondoka katika kambi za wakimbizi kwa haraka..

Aprili 08, 2024
Border
news image

Akizungumuza na wanahabari Dakika chache baada ya kukutana na viongozi wa kambi mbali mbali Pamoja na baadhi ya wakimbizi ,Gavana wa Kivu Kaskazini Peter Cirimwami ameamrisha watu wote wanao miliki silaha ,wakiwemo askari jeshi tiifu kwa serikali ,wazalendo na watu wengine kuondoka katika kambi za wakimbizi kwani kambini hakuna nafasi kwa watu wanao kuwa na silaha.

Hatua hii imechukuliwa baada ya watu wenye silaha kuanza kulipua mabomu katika makambi za wakimbizi ,kama ya Mugunga ,ambapo siku ya juma Mosi watu wa nane walijeruhiwa baada ya bomu moja kulipuka katika kambi .gavana wa Kivu Kaskazini ameomba hata hivyo wakaazi na wakimbizi kuwa watulivu kwani hivi sasa serikali ya DRC inajaribu kutafuta suluhisho.la haraka ili wakimbizi wote warudi kwenye vijiji vya.

Kwa sasa kumekuwa milipuko ya Bomu ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika kambi za wakimbizi bila kufahamu wapi zimetokea.maeneo mengi yakiwa ni Mugunga magharibi mwa Mji wa Goma ambako kuna idadi kubwa ya wakimbizi wanao kimbia vita kutoka Masisi,Rutshuru na Nyiragongo.wakimbizi ambao kwa sasa walalamikia hali ngumu ya kimaisha .kwa ukosefu wa tiba ,chakula na mahitaji mengine muhimu.

Wengi wao wakiomba kurudi nyumbani kwao kuliko kubaki ndani ya kambi .

AM/MTV DRC ONLINE