DRC

DRC EVE BAZAIBA AKERWA NA HALI MBAYA WAISHIMO WANAWAKE KATIKA KAMBI ZA WAKIMBIZI KIVU KASKAZINI.

MACHI 20, 2024
Border
news image

Waziri wa mazingira wa DRCongo EVE BAZAIBA auzunikishwa sana na hali wanayo pitia akina mama wajawazito katika kambi mbali mbali zinazo zunguuka Mji wa Goma ,BAZAIBA amesema hayo akiwa ziarani Katika Kambi ya wakimbizi wa vita vya M23 na jeshi la serikali wanao patikana katika kata la Mugunga magharibi mwa Mji wa Goma.

Akishinikizwa na ujumbe wa kanisa zinazo Sali kwa ajili ya usalama wa Taifa Bazaiba amewakabidhi msaada wa Chakula wakimbizi wa chache hasa wazee ,wajawazito na walemavu ambao Zaidi ya wiki mbili hawana chakula wakiishi Maisha magumu katika kambi.

Msaada huo ikiwa mavazi,chakula ,biscuit kwa Watoto,jerekani na vifaa vingine vya wanawake .kwa jumla wanawake wameomba kutengenezawa choo Pamoja na kupewa maji ya kunywa kwani hawana sehemu ya kunyamba na kuji saidia .kambi hiyo ikiwa na wanawake wengi waja wazito wameomba kusaidiwa na madawa .
AM/MTV DRC ONLINE