DRC

DRC BALOZI WA UTALII BI VERONIQUE KASHALA WETUNGANYI ATEMBELEA WAKIMBIZI WA VITA KIVU KASKAZINI.

MACHI 28, 2024
Border
news image

Akizungumuza na wanahabari dakika chache baada ya kukutana na Gavana makamu wa Kivu Kaskzini Bi Veronique Kashala Wetunganyi Balozi wa utalii nchini DRC aomba wananchi kuunga mkono juhudi za Rais felix Tshisekedi katika mchakato wakutafuta amani na usalama mashariki mwa Congo. Kashala anashinikizwa na Van Navel Ghislaine, mshahuri wa zamani katika serikali ilio .huu ukiwa mwezi wa kina mama ujumbe huo umesema umekuja Goma kuhitimisha mwezi wa akina mama wakiungana na sehemu ndogo ya wanawake wanao kimbia mkaazi yao kutokana na vita vya kulazimishwa .

VAN NAVEL GHISLAINE anasema mbali na Goma atawatemebelea wakaazi wa Lubero ambako alipo zaliwa kukutana na watu wanao kimbia vita vya M23 wengi wakiwa katika Miji ya Kanyabayonga ,kaina na Kirumba wakilazimishwa kuhama makaazi yao na watu wanao shikilia silaha .kwa upande wake Kashala asema ana Imani kwamba vita mashariki mwa Congo siku moja vitaisha na watu kupata amani na usalama.

Vita mashariki mwa Congo vime lazimisha ma milioni ya watu kuhama makaazi yao na kuwa wakimbizi ndani ya taifa lao kutokana na maslahi binafsi ya watu wanao sababisha wanawake na Watoto Pamoja na wazee kupoteza Maisha na wengine kuishi Maisha magumu bila kupenda kwao.

AM/MTV DRC OLNINE