DRC

Drc Goma Wakaazi Waamua Kujichukulia Sharia Mikoni Kwakuazibu Waalifu

Aprili 17, 2024
Border
news image

Wakati ambapo Mji wa Goma unaendelea kushuhudia wizi wa ngawira kwa saa za mchana kama vile usiku ,na baadae kupotea ,wakaazi waamua kujichukulia jeshiria mikononi hasa hasa kuwaua na kuchoma watu wanao kamatwa wakati wa wizi.kisa cha hivi leo nikatika kata ya Majengo ambako kijana asie julikana ameuwawa na kuchomwa moto baada ya kuiba simu swala linalo washangaza baadhi ya wachambuzi.

Tabia za kuwachoma watu baada ya kuwaua zimekuwa ziki jiri mara kwa mara Kivu kaskazini ,kutokana na serikali hasa mahakama kuwaachilia watu wanao shukiwa kutekeleza uhalifu na baadae kuachiliwa ,wakaazi washutumu vyombo vya usalama na serikali na serikali kuto wachukulia hatua watu wanao zulumu na kuwatesa wakaazi ndio sababu wameamua kujichukulia hatua.

Polisi ikijaribu kutuliza gasia bila mafanikio.Mji wa Goma kwa sasa unapitia changamoto kubwa kutokana na watu wanao zurura na silaha mikononi kila sehemu na wengine wakijikita katika wizi wa vitu.wakaazi kwa upande wao wakilaumu serikali kuwaachilia wahalifu ndio sababu waamua kujipa sharia .vitendo ambavyo ni mbaya vikiwa na kinyume sana kutokana kwamba hata wasio wizi waweza kuwawa kwa bure.

AM/MTV DRC ONLINE